• THE NATIONAL COUNCIL FOR TECHNICAL AND VOCATIONAL EDUCATION AND TRAINING
 • CENTRAL ADMISSION SYSTEM (CAS)
Login
FAQ
Frequently Asked Questions
Question 1: Nahtaji kuondoa au kujitoa kwenyenye chuo nilichoomba ili nibadili kingine nifanyaje au gharama ni ileile au inakuwa imeshakatwa gharama

Answer 1: Hakutakuwa na gharama nyingine kwenye kubadili machaguo yako na unaweza kubadili machaguo yako wakati wowote wa udahili mpaka siku ya mwisho

Question 2: Naomba kuuliza nataka kuapply kwa ajili ya upgrading ya CMT nafanyaje maana sion option ya upgrading diploma in clinical medicine

Answer 2: Baada ya kukamilisha kujaza other qualification na ukaonyesha kuwa una level 5. Kozi zote utakazo ziona ni za mwaka mmoja ambayo kimsingi ndio hiyo upgrading.

Question 3: mm nilijaza details za mwanzo ili kupata control namb nilivyomaliza kujaza nikaambiwa nixubr baada ya maxaa 24 , nikatatok kweny app, badae nimerud baada ya masaa 24, sioni hiyo control namba, je nifanyaje ili niipate mana nlishajaza details zote nikaambiwa nisubr

Answer 3: Anza kufanya usajili upya kama ulivyofanya awali mfumo utakutambua na kukurejesha pale ulipoishia.

Question 4: naweza kupata nafasi ya kuapply Nacte kwa kuunganisha index namba zangu maana nina vyeti viwili

Answer 4: Ndio unaweza. anza kufanya maombi kwa namba moja na ukikamilisha nenda kwenye profile na bofya kitufe cha secondary kisha add sit kwa kuweka namba ya pili.

Question 5: Nimeingia kwenye mfumo nimejaza taarifa zangu na baada ya hapo nikaona control number nimepewa je username na password nazipataje nikitaka kulogin Tena?

Answer 5: Ukishafanya malipo ukiwa kwenye mfumo utapewa maelekezo ya kudelea na hapo ndio utatengeneza Username na password yako.

Question 6: Jamana mimi nafanya usaili lakini kila nikifika kwenye kulipia nachagua option ya M-pesa naona maelekezo baada ya hapo naenda menu ya mpesa nalipia lakini kila nikilipia wananitumia meseji Muamala wa malipo ya serikali haujakamilika ..!! nimefanya hivyo zaidi ya mara 6 nisaidieni nifanyeje..?

Answer 6: Wasilisha tatizo lako kwenye namba za simu silizowekwa hapo kwenye mfumo kwa kutuma index number na mwaka wa kumaliza ukieleza tatizo nini.

Question 7: nimeomba chuo cha kwanza ikakamilika,, nataka kuomba chuo cha pili sipati  contor namba na niikitumia nliyo tumia kwenye kuomba chuo cha kwanz unakataa mfumo nfanyeje

Answer 7: Control Number kikisha tumika huwezi kuitumia tena. fanya machaguo tu ya chuo kingine mfumo utakuelekeza cha kufanya ili upate control number nyingine na ukishalipia ndio utwezeshwa kukamilisha uchaguzi wako.

Question 8: Nilifanya malipo kwa elfu 30...Ikagoma na pesa ikarudishwa..Nikafanya kwa elfu 10 imekubali...Tatizo nahitaji kuongeza elfu 20 iliniweze kupata chuo zaidi ya kimoja..Ile control namba inasema ishatumika..Nifanyeje kuongeza malipo?

Answer 8: Fanya machaguo mapya ya chuo kingine mfumo utakuelekeza nini cha kufanya ili upate control namba mpya na lipia kiasi utakachoulizwa na usillipe zaidi.

Question 9: Tafadhali naomba kuuliza mfumo huu ni kwa ajili ya vyuo vya afya tu

Answer 9: Ndio.

Question 10: nimefanya usaili wa awali, nimetumiwa control namba ya kulipia tsh. 10,000, lakini mpaka sasa sijatumiwa username pamoja na password, je tatizo ni nini? leo ni siku ya tano tangu nifanye usaili wa awali.

Answer 10: Rudi kwenye mfumo ujaze tena taarifa zako kama ulivyofanya mwazoni na kama utakwama tufahamishe kupitia mawasiliano yetu yaliyopo kwenye mfumo huu.

Question 11: nawezaje kuona vyuo nilivyofanyia udahili katika mlolongo ili kuhakiki udahili wangu Kama umekubaliwa

Answer 11: Ndio unaweza kuona, angalia mahala palipoandikwa "chosen programmes" unaweza kuona kama ukikamilisha application. Kama hukukamisha application unafika kwenye ukurasa wa kucagua vyuo na una sema enough choice utaona machaguo uliyokwisha kuyafanya.

Question 12: habari, nimefungua akaunti lakini nikitaka kuomba inakuja option ya vyuo vya afya tuu. nifanyeje na mm nahitaji kufanya maombi ya vyuo vya misitu?

Answer 12: Mfumo huu unapokea maombi kwa ajili ya vyuo vya afya pekee. Maombi mengine yanatumwa kwenye vyuo husika moja kwa moja.

Question 13: Nimefanya maombi kwa mara ya kwanza nikakamilisha. Nahitaji kuomba chuo kingine siipati option ya kuendelea kana ilivyokuwepo jana. Nifanyeje ili niendelee?

Answer 13: Ingia kwenye mfumo na ukiwa kwenye ukurasa wako binafsi unaweza kuongeza kozi nyingine kwa kubofya kitufe kinachoitwa "Add Choice".

Question 14: Baada ya kumaliza kujaza maombi ya chuo imenieleta hio msg hapo chini hapa ina maanisha maombi yangu yameshapokelewa? Congratulations! You have reached the end of admission application process, below is a summary of your application status. Please review it and make follow up in the places which require your attention

Answer 14: Hapa ndio mwisho na umekamilisha maombi yako.

Question 15: Nataka kurudi nyuma kuchagua priority ya course iliniletea health and allied sciences wakati mi nataka tourism niliclick bila kujua naomba mwongozo nafanyaje??

Answer 15: Mfumo huu unapokea maombi kwa ajili ya vyuo vya afya pekee. Maombi mengine yanatumwa kwenye vyuo husika moja kwa moja.

Question 16: je naweza kujua ama kuangalia katika chuo nlichoomba tuliomba watu wangapi?

Answer 16: Ndio unaweza, Ukimaliza application yako bonyeza kitufe kilicho andikwa "Chosen Programmes" mfumo utakuonyesha kwa kila chaguo kuna wanafunzi wangapi ameomba na mwishoni itaonyesha jumla.

Question 17: Tafadhali naomba kujua hatua za kufuata ili kulipa kwa M-Mpesa

Answer 17: Sehemu ambayo unaiona namba ya malipo (Control Number) Chini yake kuna aina mbalimbali ya kulipia chagua unayotaka kwa kubofya moja unayoitaka kisha itakupa jinsi ya kulipia.

Question 18: Samahani nimefanya udahili vyuo viliwi uhakika wa kupata nafasi upo ama lazima niongeze viwe vitatu?? Swali la pili. Kipndi nafanya udahili niliweka nyaraka ya cheti kimoja tu cha astashahada ,sijajua kma lazima niweke vyote hadi cheti cha sekondari naomba kufaham ili ikiwezekana nibadirishe mapema?

Answer 18: Uhakika wa kupata nafasi unategemea na ushindani kwenye kozi ulizochagua. UNashauriwa kujaza kozi zenye ushindani mdogo na unapo chagua kozi nyingi ndio unaongeza uhakika wa kupata nafasi. Nyaraka zinahitajika kwa wanafunzi waliomaliza chuo/shule zamani. Mfano waliomaliza kidato cha nne au cha sita kabla ya mwaka 1988. na waliosoma Cetificate/au Diploma kabla ya mwaka 2015 Septemba.

Question 19: 1.Je nitajuaje kuwa nimechaguliwa kujiunga na vyuo nilivyoomba?

Answer 19: Kupitia kwenye ukurasa wako binafsi ma majibu yatakaporudishwa kama ilivyo kwenye kalenda yetu.

Question 20: namna ya kupata control number nataka nilipe ili niongeze chuo kingine kwenye application yangu najaribu kutumia ile ya mara ya kwanza inakataa

Answer 20: Unaendelea na kuchagua chuo unachotaka na mfumo utaangalia kama unahitaji kulipia au la. Na kama utaona unahitaji kulipia utakutaka kutengeneza namba mpya ya malipo.

Question 21: nifanyeje ili kupata control number nyingine nataka nilipe ili niongeze chuo kingine kwenye application yangu maana najaribu kulipa kwa ile nilitumia awali inakataa

Answer 21: Unaendelea na kuchagua chuo unachotaka na mfumo utaangalia kama unahitaji kulipia au la. Na kama utaona unahitaji kulipia utakutaka kutengeneza namba mpya ya malipo.

Question 22: Nimefanya maombi mara ya kwanza niipata control ya malipo, nataka ku apply vyuo vingine natumia control hii hii au nyingine? naipatajeee? ili niweze kuendeleaaa. Ahsant

Answer 22: Unaendelea na kuchagua chuo unachotaka na mfumo utaangalia kama unahitaji kulipia au la. Na kama utaona unahitaji kulipia utakutaka kutengeneza namba mpya ya malipo.

Question 23: samahani mm nimelipia sh 10000 lakini baada ya kulipia chuo nilichokuwa nakitafuta sijakiona nilitaka chuo cha mbeya cha sheria lakni huku nimekuta vya afya samahani nafanyaje

Answer 23: Maombi yanayotumwa kupitia mtandani na ya vyuo ya afya pekee. Maombi mengine yote yanatumwa kwenye vyuo husika.

Question 24: Hello Nimefanya online kupitia online admission ,Nimeomba vyuo vitano lakini vyuo vitatu tu ndo control number ilitoka nikalipia lakini viwili control number haikutoka lakin system ikaniruhusu kuendelea..swali langu maombi yangu yatakua yamefika yote?

Answer 24: Maombi yako yamepokelewa. Gharama ya maombi ni shiling elfu kumi kwa chuo ila ikifiaka elfu thelathini unaruhusiwa kuomba mpaka vyuo vitano.

Question 25: Nilimeto kwenye mfumo ili nilipe na baada ya kulipa sipati link ya kuendelea tena. Nimeshalipia

Answer 25: Kama hukumalizia usajili anza kufanya tena usajili mfumo utahakiki malipo yako na kukuruhusu kuendelea na maombi yako.

Question 26: Swali langu ni:mwaka jana nilituma maombi(udahili) wa vyuo takribani ni vyuo vitatu cha kusikitisha sikupata nafasi katika vyuo hivyo vyote mwaka huu pia nimetuma je, nawezaje kupata uhakika kuwa nitapata nafasi katika vyuo hivyo? Ahsanten

Answer 26: Uchaguzi unategemea ushindani kwa kuangalia yafuatayo;-

 • 1. Ufaulu wako kwa kuzingatia masomo ya Bailogia,Kemia, Fizikia Hisabati na Kingereza. Na waombaji watapagwa kwa ufaulu kuanzia aliyefaulu zaidi kuwa juu na kuendelea.
 • 2. Nafasi zilizopo kwenye kozi husika.
  Kwa hiyo basi unatakiwa kuchagua kozi ambazo zina ushidani mdogo kama ufaulu wako ni wa chini. Mfumo unakuonyesha kila kozi unayoichagua kuwa ina waombaji wangapi.

 • Question 27: Mm nataka kuingia tena na ni apply chuo kingine lakn session imeisha muda wake na pia nimesahau password yangu na nikienda kwenye forgot my password naandikiwa kuwa payment code cyo sahihi jaman naomba mnisaidie ili niweze ku apply chuo kingine

  Answer 27: Usajili wako ukikamilika mfumo unakupatia username na password kwa njia zifuatazo.

 • 1. Inakuonyesha mara tu unapo maliza usajili pale pale kwenye mfumo na kukupa maelekezo ya kuinakili sehemu kwa matumizi ya baadae
 • 2. Inatumwa kwa sms kwenye simu uliyo itumia wakati wa usajili
 • 3. Inatumwa kwenye email uliyo isajili kwenye mfumo

 • Na ikiwa njia zote hizi kwa namna moja au nyingine hakuzingatiwa unaweza kuomba tena hiyo password kwa kutumia link ya forget password inayopatikana kwenye ukurasa wa login. kwa kuweka risiti ya malipo uliyofanya wakati wa usajili, username yako ambayo ni namba ya kidato cha nne ikiungwanishwa na mwaka uliohitimu, barua pepe uliyotumia na simu uliyoisajili hapo awali na mfumo utatuma tena password kwenye namba ya simu na barua pepe.

  Question 28: Namna ya kupata mwongozo wa kulipia gharama za kufanya application kwa kila institution

  Answer 28: Garama za malipo zimewekwa kwenye ukurasa wa kwanza wa mfumo huu. Ambapo ni shilingi elfu kumi kwa chuo kimoja na kila ukiongeza chuo utaongeza elfu kumi. Na malipo yakifikia elfu thelathini unauwezo wa kuchagua mpaka vyuo vitano.

  Question 29: Najaribu kujisajili kwa mara ya kwanza lakn naambiwa index namba siyo sahihi lakin kiuhalisia index namba na mwaka wa kuhitimu vipo sahihi msaada tafadhali

  Answer 29: Kuna mambo kadhaa yanaweza kuwa sababu ya hili.

 • 1. Umekosea kuandika namba yako ya mtihani wa kidato cha nne, unashauriwa kuangalia na kuiandika kwa usahihi
 • 2. Matokeo ya mtihani yamezuiliwa na Baraza la taifa la mitihani kwa sababu mbalimbali
 • 3. Kuna matatizo ya kiufundi kwenye mtandao, Unashauriwa kujaribu tena baadae/wakati mwingine
 • Question 30: najaribu kujisajili kwa kuweka index namba na mwaka lakini mfumo unaniambia invalid index number or examination year

  Answer 30: Kuna mambo kadhaa yanaweza kuwa sababu ya hili.

 • 1. Umekosea kuandika namba yako ya mtihani wa kidato cha nne, unashauriwa kuangalia na kuiandika kwa usahihi
 • 2. Matokeo ya mtihani yamezuiliwa na Baraza la taifa la mitihani kwa sababu mbalimbali
 • 3. Kuna matatizo ya kiufundi kwenye mtandao, Unashauriwa kujaribu tena baadae/wakati mwingine
 • Question 31: Nimeshindwa kupata control namba.

  Answer 31: Namba ya malipo (Control Number) inapatikana baada ya kufanya usajili kwa kuweka taarifa za awali. Na inachukua mpaka dakika tano kuipata baada ya kupokea hizo taarifa. Isipotokea baada ya masaa ishitini na nne. wasiliana na wataalamu wetu kwa namba ########## au ########### siku za kazi kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi jioni.

  Question 32: Nimelipia ada ya udahili lakini hakuna kilichofunguka.

  Answer 32: Malipo yakisha lipwa baada ya kupata namba ya malipo unatakiwa kuwepo kwenye ukurasa wa kutengeneza ankra. Na kama ulishaondoka fanya usajili upya kama ulivyofanya mara ya kwanza na mfumo utaangalia kama malipo yamefika na kukupeleka sehemu inayofuata.